HOSPITALI ZA RUFAA ZA MIKOA (TEMEKE, MWANANYAMALA NA AMANA) ZAPEWA MAUA YAO

Posted on: November 19th, 2023

HOSPITALI ZA RUFAA ZA MIKOA (TEMEKE, MWANANYAMALA NA AMANA) ZAPEWA MAUA YAO

Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dkt. Godwin Mollel, amefanya ziara ya kukagua utoajia wa huduma katika Hospitali za Rufaa za Mikoa za dar es salaam leo. katika ziara ya hiyo, Mhe. Dkt. Godwin mollel ameweza kutembelea maeneo mbalimbali ya hospitali hizo ikiwemo jengo jipya la huduma za dharula(EMD), jengo jipya la radiolojia na kujionea machine mpya ya CT Scan katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke. Pia Mhe. Dkt. Mollel ameweza kupita katika jengo la huduma za dharula(EMD) na kitengo cha usafishaji damu (dialysis) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.

Katika mazungumzo yalifanyika mara baada ya ziara hiyo Mhe. Dkt. Mollel amesema kuwa, amefurahishwa na huduma bora zinazotolewa katika hospitali hizo na kupongeza jitihada zinazofanywa na waganga wafawidhi pamoja na uongozi wa hospitali hizo, na kusema kuwa hakika atafikisha salamu kwa waziri wa afya mhe. Ummy mwalimu kuwa hospitali hizo zipo katika viwango bora za huduma.

“nikirudi nitafikisha salamu hizi kwa Mhe. Ummy na kumwambia asiwe na wasiwasi kabisa kuhusu Hospitali za Rufaa za Mikoa kwani zipo vizuri sana”

Aidha Mhe. Dkt. Mollel amesisitiza kuhakikisha timu ya uendeshaji wa hospitali za mikoa kuhakikisha wanadumisha utoaji wa huduma bora kwa wateja (Good customer service) wakati wa kuhudumia wagonjwa kwa kutoa huduma zinazostahili kama ambazo wao watumishi wangependa kuzipata.

Kwa upande wa Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikioa, Dkt. Joseph Kimaro wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dkt. Zaveri Benela wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala na Dkt. Bryceson kiwelu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana wametoa shukrani pamoja na pongezi kwa serikali ya awamu ya sita kwa wekeza na kuongeza jitihada za kuboresha huduma za afya nchini