SIKO SELI(SICKLE CELL) NI NINI? JE UNAFAHAMU KIPIMO SAHIHI CHA SIKO SELI?
Posted on: October 19th, 2023
Selimundu(Sickle cell) ni Ugonjwa wa kurithi, unaotokana na uwepo wa seli za damu zenye umbo tofauti na la kawaida. Mtu mwenye tatizo hili huwa na changamoto ya kupungukiwa damu mara kwa mara , maumivu ya kichwa, viungo, pamoja na misuli.
Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia wizara ya Afya za kutoa elimu kwa Umma juu ya ugojwa wa selimundu (sickle cell) kutana na mtaalamu wa maabara Evelyne Mbaga kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke akielezea kipimo kinachopatikana hospitalini hapo chenye uwezo wa kutambua kama mtu anatatizo hilo la selimundu.
Kipimo hicho kwa lugha ya kitaalamu kinaitwa Hb Electrophoresis, kinatumika kuthibisha ugonjwa huo kwa kutoa asilimia ya kila aina ya hemoglobini ikiwemo hemoglobini ya selimundu
Naye, Evelyne Mbaga ametoa ushauri kwa wana ndoa ambao wanatarajia kufunga ndoa, kuhakikisha wanafanya uchunguzi wa kutambua kama wana chembe chembe za selimundu zitakazo pelekea mtoto wao kuzaliwa na ugonjwa wa selimundu, kwani itarahisisha namna ya kumuangalia na kufuatilia afya yake.